YANGA SC MAMBO SAFI KWA KABAMBA TSHISHIMBI

KIUNGO mpya wa Yanga, Kabamba Tshishimbi juzi Jumatano amefanyiwa vipimo vya afya na kufanikiwa kufuzu na sasa amebakiza hatua moja kusaini mkataba wa miaka miwili.

Kiungo huyo raia DR Congo amefanyiwa vipimo hivyo juzi mbale ya madaktari watatu wakiongozwa na aliyekuwa Daktari wa Yanga, Nassoro Matuzya.

Zoezi hilo ambalo lilisimamiwa na mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Yanga, Hussein Nyika Kabamba alionekana kuwa fiti kiasi cha kusifiwa na madaktari hao.

“Tunakaribia kumalizana na Kabamba, kuna zoezi ambalo tulikuwa tunalifanya juzi la kupima afya ambalo amefuzu na sasa tunajipanga kamalizana naye,” alisema Nyika.


Tayari kikosi cha Yanga kimeshaondoka juzi mchana kuelekea kambini mkoani Morogoro ambapo endapo kiungo huyo atamaliza kila kitu atasafirishwa haraka kuungana na wenzake.

No comments