YANGA YATAMBA KUIZIDI UJANJA SIMBA USAJILI WA WACHEZAJI KIKOSI CHA TIMU YA TAIFA

YANGA wamedai kutarajia kuwazidi kete Simba kwa kufanya usajili wa maana kwa wachezaji wanaocheza katika kikosi cha timu ya Taifa Stars kwa msimu ujao wa Ligi Kuu na mashindano mengine.

Kikosi cha Taifa Stars ambacho kipo Afrika Kusini kushiriki michuano ya COSAFA na inasemekana mabosi wa Yanga wamepanga kuchomoa vifaa ambao wapo katika mazungumzo na baadhi ya wachezaji nyota.

Yanga ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara wanaendelea kusuka kikosi chao kimyakimya kwa kuhofia hujuma kutoka kwa wapinzani wao wa soka wakiwamo watani wao wa jadi, Simba.

Akizungumza na saluti5, mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Yanga, Husein Nyika alisema kuna wachezaji wamepanga kuwasajili katika timu ya taifa na wanasubiri wachezaji watakaporejea nchini wamalizane nao.

Nyika alisema falsafa yao ya msimu huu ni kusajili wachezaji chipukizi zaidi ambao wataitumikia klabu hiyo kwa miaka mitano au sita mbele.

“Siwezi kuweka wazi usajili wetu kwa sababu ukisema tunamsajili mchezaji fulani utasikia klabu nyingine inamtaka na kutibua mipango yetu wewe subiri timu itakaporejea utaona kazi,” alisema Nyika.


Tayari Yanga wamesajili wachezaji wapya Abdallah Haji, Shaibu Ninja kutoka Jang’ombe, Zanzibar Pius, Buswita (Mbao FC), huku wengine kama Donald Ngoma, Amis Tambwe na Haji Mwinyi wakiongezewa mikataba.

No comments