YOUNG KILLER ATAJA VIGEZO ANAVYOVIZINGATIA ATAKAPOPATA LEBO YA KUREKODI

RAPA Erick Msodoki maarufu kama "Young Killer" ametaja vigezo anavyozingatia pale inapotokea lebo ya kumsimamia na kusema kwamba hataangalia ukubwa wa lebo bali jinsi atakavyoweza kutoka kimuziki.

Msodoki alisema sio lazima lebo iwe na jina ila iwe na uwezo wa kufanya kazi katika kiwango kikubwa, pia lazima iwe na hela kwa sababu muziki wa sasa umekuwa biashara na unahitaji hela.


“Nimekuwa nikifanya kazi mwenyewe lakini nimekuwa nikipigania sana kile kidogo ninachopata na kuweza kukiweka katika muziki wangu," alisema rapa huyo ambaye kwa sasa anafanya vyema na ngoma yake ya "Unanionaje".

No comments