MSANII wa muziki wa bongofleva, Z Anto amesema hajawahi kuwaza wala kutamani kufanya kolabo na nyotab wa muziki huo wanaofanya vyema kwa sasa, Ali Kiba na Diamond Platnumz.

Z Anto alisema hataki kufanya kolabo na mmoja wa mastaa hao kwa sababu hahitaji kuegemea upande wowote.


“Sijawahi kuwaza kufanya nao kolabo kwani ni watu ambao wameshajitengenezea njia zao na mimi sitamani kuzipita bali kama Diamond alipita kushoto na Ali Kiba akapita kulia, basi mimi nataka nipite katikati nifanikishe mambo yangu,” alisema.
USISAHAU KUBONYEZA SUBSCRIBE HAPO
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac