ZANZIBAR STARS KAMA KAWA LEO DDC KARIAKOO

KAMA kawa baadae leo bendi ya mipasho iliyorejea kwenye gemu kwa kishindo kikubwa, Zanzibar Stars Modern Taarab itaangusha burudani zake ndani ya DDC Kariakoo, imefahamika.

Bosi wa Zanzibar Stars, Juma Mbizo amesema kuwa saa 3:30 usiku vijana wake watakuwa tayari wameanza kudondosha mzigo mdogomdogo huku kiingilio kikiwa ni sh 3 ,000 kwa watakaozama ukumbini kabla ya saa nne usiku.  


“Tunawaomba mashabiki waendelee kutusapoti kwa kuzidi kufika kwa wingi leo kwenye shoo hii ambayo tumeiboresha zaidi na tunawaahidi watakaohudhuria kuwa watafurahi na roho zao kwa raha za burudani tutakazowapa,” amesema Mbizo.

No comments