ZANZIBAR STARS KUUNGURUMA USIKU HUU DDC KARIAKOO …pata picha 10 za show ya Jumanne iliyopita


Ujio mpya wa Zanzibar Stars Modern Taarab ulioanza kwa kishindo Jumanne iliyopita, usiku huu utaendelea tena ndani ya ukumbi wa DDC Kariakoo, jijini Dar es Salaam.

Kundi hilo ambalo bado linasukwa upya baada ya kupotea kwenye ‘gemu’ kwa takriban miaka 10, limeutangaza ukumbi wa DDC Kariakoo kama ngome yao ya kila Jumanne.

Wakazi wengi waliojitokeza DDC kariakoo Jumanne iliyopita, walionekana kukunwa na ujio huo mpya wa Zanzibar Stars ambayo hata hivyo bado inatumia wasanii wengi waalikwa kutoka bendi nyingine.

Bosi wa bendi hiyo Juma Mbizo aliiambia Saluti5 kuwa kwa sasa wanaanza kwa kutumia wasanii waalikwa waliowahi kuitumikia Zanzibar Stars huko nyuma.

“Ndio maana tumeichagua Jumanne ambayo bendi nyingi huwa mapumzikoni, hivyo ni rahisi kwetu kuwapata wasanii wa zamani wa Zanzibar Stars,” alisema Mbizo.

Bosi huyo wa Zanzibar Stars akaongeza kuwa baadae watatangaza safu ya wasanii wao ingawa mfumo wa kuwa na wasanii waalikwa utakuwa wa kudumu.

Miongoni mwa wasanii waalikwa waliojitokeza wiki iliyopita ni pamoja na Hadija Yussuf, Mosi Suleiman, Zubeda Mlamali, Mwamvita Shaibu, Issa Kamongo na Bi Mwanahawa Ally.

Pata picha kadhaa za onyesho la kwanza la Zanzibar Stars ndani ya DDC Kariakoo Jumanne iliyopita.

 Fikirini Urembo akicharaza solo gitaa
 Issa Kamongo na Hadija Yussuf wakiimba wimbo "Udugu Hazina Yetu"
 Omar Kisila kwenye kinanda
 Mosi Suleiman wa Jahazi naye alikuwepo
 Mussa Mipango na bass lake
 Bi Mwanahawa Ally akikonga nyoyo za mashabiki wa Zanzibar Stars
 Kutoka kushoto ni Mosi Suleiman, Mwanamkuu Zayumba na Zubeda Mlamali wakiwa kwenye safu ya uitikiaji
Waimbaji wa Ogopa Kopa Mwamvita Shaibu na Zena Mohamed (kulia) nao walishiriki ononyesho la Zanzibar Stars
Zubeida Mlamali wa Jahazi akishiriki onyesho la Zanzibar Stars


No comments