ZANZIBAR STARS WAONYESHA MWANZO MZURI DDC KARIAKOO

JUMANNE iliyopita ukumbi wa DDC Kariakoo, jijini Dar es Salaam ulionekana kuwa na ‘joto’ kutokana na mamia ya mashabiki waliofurika kuushuhudia ujio mpya wa bendi ya Zanzibar Stars Modern Taarab.

Shoo ya Jumanne ndani ya DDC Kariakoo ilikuwa ni ya kwanza kwa bendi hiyo iliyorejea upya, baada ya ile maalum iliyopigwa siku ya sikukuu ya Idd Mosi ndani ya Dar Live sambamba na wasanii wa bongofleva.

Saluti5 iliyekuwepo ukumbini kuanzia mwanzo hadi mwisho wa shoo hiyo, ilishuhudia namna mastaa kibao wanaonogesha bendi iliyorejea upya hivi karibuni wakichangia kuwacharusha mashabiki wa mipasho.

Kila wimbo ulioangushwa ulionekana kuwakuna zaidi mashabiki ambao wengi wao walionekana kutokauka katikati kucheza, huku wengine wakipanda jukwaa la wasanii kwenda kumwaga noti kutokana na kupagawa zaidi.


Kwa mujibu wa bosi wa Zanzibar Stars, Juma Mbizo, bendi hiyo itakuwa ikiungurumisha burudani ndani ya ukumbi huo kila wiki katika siku za Jumanne.

No comments