ZIDANE APOTEZEA KIPIGO CHA BARCELONA

KOCHA  wa Real Madrid, Zinedine Zidane  ni kama amekipoteza kipigo walichokipata majuzi dhidi ya mahasimu wao  Barcelona  katika michuano ya Kombe la Mabingwa wa Kimataifa baada ya kusema kwamba  anachokiangilia ni mchezo wao ujao wa michuano ya  UEFA Super Cup  dhidi ya  Manchester United.

Katika mchezo huo ambao ulikuwa ni wa kirafiki uliofanyika mjini Miami nchini Marekani Reaa Madrid  walijkuta wakinyukwa  kwa mabao  3-2.

Bao la dakika 50 lililowekwa kimiania  na staa Gerard Pique ndilo lililowafanya  Barcelona  kupata ushindi wa kwanza wa  Clasico msimu huu  wa  2017-18  na huku likiwaacha Real  Madrid  bila kupata ushinndi wowote baada ya kucheza mechi tatu katika mashindanio hayo.

Hata hivyo pamoja na matokeo hayo yanaonekana kutomshutua , Zidane  baada ya kusema kuwa kilichpo kicvhwani mwaka ni kuhusu mechi hiyo ya ufunguzi wa ligi dhidi ya Man Utd ambayo itakapigwa mjini  Skopje nchini Macedonia, Agosti 8 mwaka huu.

"Haya ni maandalizi ya msimu ujao na nina uhakika ni matoke ambayo hatukuyatarajia ,lakini hii haiumizi kichwa ,"alisema  Zidane ambaye kikosi chake keshokutwa kitakuna na timu ya  MLS All-Stars mjini  Chicago kabla ya kurejea kwenye michuano hiyo ya Ulaya.


 "Jambo la muhimu na la msingi ni kujiweka sawa  kwa ajili ya mechio hiyo ya Agosti 8. Tutaona kitu kizuri kuanzia hapo na bvilevile kile ambacho sikitaki na inatubidi kuwa na subira, tujitume na kuwa tayari kwa ajili ya mechi hiyo ya  UEFA Super Cup,”aliongeza Mfaransa huyo.

No comments