2FACE IDIBIA AKANA KUBUGIA FEDHA ZA MISAADA YA WATOTO

STAA wa muziki wa taratibu, 2Face Idibia amekanusha vikali madai ya kujiingizia fedha kwa njia ya utapeli akishtumiwa kula fedha za misaada ya watoto wenye matatizo ya akili.

Staa huyo amekuwa akitembeza bakuli kwa wahisani mbalimbali ili kutunisha mfuko wa kusaidia watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu wakiwemo wenye matatizo ya akili.

Mpangu huo aliuanza ukiwa na kipaumbele cha kugusa watoto ambao wameathiriwa na kundi la Boko Haram linalosumbua serikali ya Nigeria.

“Inakatisha tamaa kidogo kwani nilitarajia kuungwa mkono katika jitihada zangu za kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu lakini badala yake zimeibuka shutuma,” alisema rapa huyo.


“Siwezi na wala sina mpango wa kujinufaisha na fedha za wahisani, hii ni wazo nililokuwa nalo muda mrefu,” aliongeza.

No comments