40 YA SHABAAN DEDE NI JUMAMOSI HII


Kisomo cha kutimiza siku 40 za kifo cha mwimbaji Shaaban Dede, kitafanyika Jumamosi hii August 12, jijini Dar es Salaam.

Hamad Dede ambaye ni mtoto wa marehemu, ameiambia Saluti5 kuwa kisomo hicho kitafanyika Kariakoo mtaa  Congo na Msimbazi wa saa 7 mchana.

Shaaban Dede aliyekuwa nguzo ya Msondo Ngoma, alifariki dunia Julai 7 katika hospitali ya taifa ya Muhimbili na kuzikwa makaburi ya Kisutu Julai 7.

Dede ambaye pia aling’ara na bendi za Mlimani Park “Sikinde”, Bima Lee na OSS, alifariki kutokana  na maradhi ya sukari pamoja na figo.

No comments