ABDU KIBA AMKINGIA KIFUA KAKA YAKE LAWAMA ZA UKIMYA WA NGOMA MPYA

MSANII Abdu KIba amemkingia kifua kaka yake, Ali kiba wakati huu ambao mashabiki wanamwandama kuhusu kutoa ngoma mpya.

Mwimbaji huyo amekiambia kipindi cha "XXL" cha Clouds Fm kuwa hilo wanalichukulia kama changamoto ila kitu ambacho hawakipendi ni kuhusishwa na "team" za kimuziki au kuonekana kushindana na watu fulani.

“Sisi tunachukulia changamoto kwa sababu sisi hatushindani tunafanya kazi na hatujaona bado wa kushindana nao, hakuna mtu wa kushindana na sisi, yaani sijamuona wa kushindana naye na hakuna wa kushindana na sisi na sisi hatushindani,” amesema Abdu Kiba.


Wiki iliyopita Abdu Kiba alikaririwa akisema ngoma mpya ya Ali Kiba ipo mbioni kutoka.

No comments