AC MILAN YAANZA KUTETA NA SUSO ILI KUIKATILI TOTTENHAM INAYOMWINDA

TIMU ya AC Milan imeanza kuteta na nyota wao ambaye anawindwa kwa udi na uvumba  na klabu ya  Tottenham, Suso  ili kuona kama watampa mkataba mpya.


Mkataba wa sasa wa staa huyo raia wa Hispania, unamalizika miaka miwili ijayo na majira haya ya joto amekuwa akimezewa mate na Spurs ili kujaribu kumrejesha  kiungo huyo mshambuliaji nchini  England ambako amewahi kuishi wakati akiichezea  Liverpool.

No comments