ADHABU YA KUFUNGIWA MECHI TANO KUMKIMBIZA RONALDO REAL MADRID?

MSHABULIAJI wa timu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo ameonekana kuchoshwa na maisha ya Hispania hivyo kuacha maswali kuwa huenda akawa na mpango wa kutaka kuondoka.


Kitendo cha kufungiwa mechi tano baada ya kumsukuma mwamuzi kwenye mechi dhidi ya Barcelona kimeonekana kumkera zaidi mshambuliaji huyo raia wa Ureno ambaye rufaa yake ilitupiliwambali.

No comments