AJIB AGOMA KUIZUNGUMZIA SIMBA SC

MSHAMBULIAJI mpya wa timu ya Yanga, Ibrahim Ajib amesema kuwa kwasasa asingependa kuendelea kuzungumzia masuala ya Simba kwa sababu sio klabu inayommiliki tena.

Mshambuliaji huyo amesema yeye ni mali ya Yanga hivyo masuala yote yanahusu Simba ni vyema wangeulizwa viongozi wa klabu hiyo.

“Naomba ifahamike kuwa mimi ni mchezaji halali wa Yanga hivyo kama ni suala la mimi kuhusiana na namna ambavyo niliondoka Simba nadhani wanaopaswa kuhojiwa ni viongozi na sio mimi,”alisema mshambuliaji huyo.

“Akili yangu kwa sasa ni kuona namna gani naweza kuisaidia klabu kutetea ubingwa wa Ligi Kuu bara pamoja na michuano ya kimataifa, hivyo sina jambo ninaloweza kuongea kuhusu Simba,” aliongeza.


Ajib amekuwa kwenye midomo ya wanahabari tangu atue Jangwani kutokana na aumuzi wake wa kuachana na klabu ya Simba na kujiunga na Yanga ambao walifika dau alilotaka.

No comments