AJIB APANIA KUWAZIBA MIDOMO MASHABIKI WA SIMBA SC KIPUTE CHA NGAO YA HISANI

MSHAMBULIAJI wa Yanga Ibarihimm Ajib amesema kuwa katika mechi ya Ngao ya Hisani ikiwa atafanikiwa kuanza katika kikosi cha kwa atacheza kufa na kupona ili kuhakikisha anawaziba mdomo waliokuwa wakibeza na kuanza kuandika historia ya kubeba mataji akiwa chini ya utawala mwingine.

Ajib utakuwa mchezo wake wa kwanza kuchezea Yanga dhidi ya Simba ambapo ameapa kucheza soka la kiwango cha juu katika mtanange huo.

“Ni kweli Simba wamefanya usajili mzuri msimu huu lakini kwa jinsi tulinyojipanga naona kila dalili ya kubeba Ngao ya Hisani nikiwa na jezi ya Yanga kwa mara ya yangu ya kwanza,” alisema Ajib.

“Suala la nani ataanza kwenye kikosi cha kwanza ni kocha pekee yake anajua lakini endapo nitapata nafasi ya pekee kwangu kuonyesha kile ambacho ninacho maana najua yanazungumzwa mengi zinapokaribia mechi hizi,” aliongeza Ajib.

“Kwangu litakuwa jema na kubwa kuanza kuichezea na yanga nikiwa na taji mkononi” alimaliza mshambuliaji huo.


Yanga ilifanikiwa kumsajili mshambuliaji huyo baada ya kutokea hali ya vuta nikuvute ya kimaslahi kati yake na klabu ya Simba.

No comments