ALEX IWOBI NJE TIMU YA TAIFA NIGERIA

STRAIKA Alex Iwobi, amejiondoa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Nigeria kutokana na majeraha yanayomkabili na huku nafasi yake ikichukuliwa na Aaron Samuel.

Hadi sasa msimu huu Iwobi ameshacheza dakika 11 za mechi za Ligi Kuu England na hivyo atazikosa mechi mbili hizo za kufuzu fainali za Kombe la Dunia dhidi ya Cameroon kutokana na matatizo ya misuli ya nyama za paja ambayo yalimfanya pia Jumapili aikose mechi  ya Arsenal dhidi ya Liverpool.

Mbali na kuzikosa mechi hizo majeraha hayo kwa staa huyo mwenye umri wa miaka 21, pia yanaonekana kuathiri mchakato wake wa kwenda kujiunga na klabu ya Galatasaray alipo mjomba wake, Jay-Jay Okocha.


Katika michezo hiyo ya kufuzu fainali za Kombe la Dunia, Nigeria ambao ndio wanaoongoza kundi lao baada ya kucheza mechi mbili wataikaribisha Cameroon Septemba mosi katika mji wa Uyo, kabla ya kufunga safari kwenda Yaounde siku tatu baadaye.

No comments