ALLY MAYAI ATAKA NGUVU IELEKEZWE KATIKA KUWAUNGA MKONO WALIOSHINDA UCHAGUZI TFF

BAADA ya uchaguzi mkuu wa TFF kumalizika na kupata viongozi wapya watakaohudumu kwa miaka minne, wadau wengi walikuwa na shauku ya kutaka kusikia chochote kutoka kwa washindi pamoja na wale walioshindwa huku Ally Mayai akisema suala hilo sasa inabidi lifungwe na nguvu ilielezwa katika kuwaunga mkono washindi.

“Uchaguzi umekamilika kilichobaki ni sisi kuwaunga mkono waliochaguliwa kwa sababu lengo la wote lilikuwa ni kwa ajili ya manufaa ya mpira wa Tanzania,” alisema Ally Mayai.

“Sisi ndio waasisi wa mpira wa miguu na dhana ya ‘fair play’ unafungwa magoli 9-0 na unaondoka na kwenda kumuunga mkono aliyekufunga mnakaa pamoja na kunywa mvinyo,” aliongeza Ally Mayai.

“Tunashukuru sana wajumbe kwa uchaguzi na tumemaliza vizuri umesimamia uchaguzi ulikuwa huru na haki, mambo yamekwenda vizuri watu wamezungumza mambo ya maana”alimaliza.


Mdau huyo wa soka aliwahi kuwa nahodha wa kikosi cha Yangamiaka ya nyuma kabla ya kuangukia kwenye masuala ya uchambuzi wa michezo huku pia akitoa ushauri wa kitaalamu kuhusiana na masuala ya fedha.

No comments