AMBER ROSE AJIPANGA KUFANYA UPASUAJI WA MATITI ILI KUTENGENEZA SHEPU YA KIFUA

MWANAMITINDO mwenye vituko nchini Marekani, Amber Rose yupo kwenye mkakati mzito wa kutaka kufanya upasuaji wa matiti yake ili kubadili muonekano wake.

Ambaer Rose ametuma ujumbe kwenye mitandao ya kijamii akisaka ushauri kabla ya kifikia uamuzi huo wa kubadili mwonekano wake.

“Nataka kubadili kifua changu lakini je umewahi kuwaza juu ya maumivu wakati wa upasuaji,” ilisomeka sehemu ya taarifa iliyotumwa na mrembo huyo.


Amber amekuwa miongoni mwa mastaa wenye vituko na kusababisha wakati mwingine asiweze kudumu kwenye mahusiano ya kimapenzi na mastaa ambao amekuwa akitoka nao.

No comments