AMITIE MUSICA BENDI BORA MOMBASA …kuzindua albam mpya yenye rumba kali


Hakuna ubishi kuwa hii ndio bendi yenye mashabiki wengi zaidi jijini Mombasa, Kenya. Hii ni AMITIE MUSICA yenye umri wa zaidi ya miaka 20.

Bendi hii ambayo inaongozwa na Crispin Tambwe imekuwa ikipata kazi nyingi kiasi cha kulazimisha igawanyike mara mbili - Amitie Musica A na Amitie Musica B zote zikiwa chini ya Tambwe (pichani juu aliyevalia nyeupe).

Kwasasa bendi hii iko mbioni kuzindua albam mpya inayokwenda kwa jina la “Hoki Hoki” yenye jumla ya nyimbo 12.

Ndani ya albam hiyo utakutana na nyimbo tatu za rumba na tisa za sebene la mwendokasi.

Amitie Musica A Club Zeituni, Bamburi, Mombasa kila Jumamosi huku Amitie Musica B wakipatikana Leisure Club kila Jumamosi wakati siku zingine ni za kazi mbali mbali katika maeneo tofauti.

Imeandikwa na Prince Kinmedia, Nairobi Kenya.

No comments