ARSENAL KUSUKA AU KUNYOA KWA ALEX OXLADE-CHAMBERLAIN …imuuze sasa hivi au aondoke bure msimu ujao

Arsenal iko hatarini kumpoteza winga wake Alex Oxlade-Chamberlain na pengine italazimika kumpiga bei mwezi huu.

Nyota huyo wa kimataifa wa England yuko katika mwaka wa mwisho wa mkataba wake na inaaminika atakataa ofa ya dili jipya ambalo lingemwingizia pauni 180,000 kwa wiki.

Alex Oxlade-Chamberlain mwenye umri wa miaka 24 anawaniwa na Chelsea na Liverpool na sasa Arsenal itabidi iamue moja - kuumuza mwezi huu au aondoke bure msimu ujao.No comments