ARSENAL YADAIWA KUPIMA UPEPO KWA KIUNGO JEAN MICHAEL SERI WA NICE

TIMU ya Arsenal inaripotiwa kuwa inapima upepo jinsi ya kumnasa kiungo wa Nice, Jean Michael Seri, kabla ya dirisha la usajili msimu huu halijafungwa.


 Mtandao wa ESPN FC uliripoti kuwa Seri mwenye umri wa miaka 26, alianza kung’ara tangu alipojiunga na Nice mwaka 2015 akitokea katika timu ya Pacos de Ferreira ya nchini Ureno na kwamba kwa mara kadhaa msimu uliopita  Arsenal  walikuwa wakimfuatilia baada ya kuiwezesha timu hiyo kumaliza ligi ya Ufaransa ikiwa nafasi ya tatu na kufanikiwa kufuzu kucheza michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

No comments