ARSENAL YATWAA NGAO YA HISANI, YAIBANJUA CHELSEA KWA MATUTA


Arsenal imetwaa Ngao ya Hisani baada ya kuitungua Chelsea kwa matuta kwenye mchezo  uliochezwa Wembley.

Katika mchezo huo ulioisha kwa sare ya 1-1 ndani ya dakika 90 za kawaida, Arsenal ikakwamisha mikwaju minne ya penalti huku Chelsea wakipata moja.

Waliokosa penalti kwa upande wa Chelsea ni mshambuliaji mpya Alvaro Morata na kipa Thibaut Courtois huku ile pekee iliyokwenda wavuni ikipigwa na beki Gary Cahill.

Penalti za Arsenal zikafungwa na Theo Walcott,  Nacho Monreal,  Alex Oxlade-Chamberlain, Olivier Giroud.

Victor Moses aliitanguliza Chelsea dakika ya 48 lakini Sead Kolasinac akaisawazishia Arsenal kunako dakika ya 82 baada ya kutumia vizuri faida ya wapinzani wao kuwa pungufu kufuatia kadi nyekundu aliyolambwa Pedro Rodriguez dakika ya 80.

No comments