ASLAY AANIKA SABABU YA KUACHIA NGOMA MFULULIZO

MSANII wa Bongo Fleva, Aslay Isihaka “Dogo Aslay” ameweka wazi sababu zilizomfanya atoe nyimbo nyingi kwa wakati mmoja.

Aslay ambaye sasa anatamba na wimbo wa "Baby" hivi karibuni ametoa nyimbo tano mfululizo.

Alisema chanzo cha kutoa nyimbo hizo ni kupotea kwa "flash" ya kazi zake, kitu kilichosababisha zianze kuvuja.

“Sikutaka kutoa kazi kama ilivyokuwa, lakini imesababishwa kwa kupotea kwa flash ya kazi zangu na kupelekea kazi kuanza kuvuja mtaani,” alisema Aslay.”

Alisema ilibidi kufanya hivyo sababu sasa ni msanii anayejitegemea, baada ya kuondoka kwenye kundi la Yamoto Band, hivyo anahitaji kuwa na nyimbo nyingi ambazo zitamsaidia kwenye shoo.

“Siwezi simama kwenye jukwaa nikaanza kuimba nyimbo za Yamoto Band wakati sipo huko, hivyo nahitaji kuimba nyimbo zangu mwenyewe," alisema.


No comments