ATLETICO MADRID YAMWAMBIA DIEGO COSTA AKAOMBE MSAMAHA CHELSEA


Diego Costa ameambiwa na klabu ya Atletico Madrid kuwa ahakikishe anamalizana kwa amani na Chelsea ili klabu hiyo ya Hispania iweze kumsajili.
Hii inamaanisha kuwa nyota huyo sasa yupo kwenye shinikizo la kurejea England kumaliza matatizo yake na klabu yake.
Vilabu hivyo viwili viko mazungumzoni kwaajili ya usajili wa Costa ingawa bado havijaafikiana kuhusu bei.
Chelsea inataka pauni milioni 50 lakini Atletico ipo tayari kulipa nusu tu ya bei hiyo.

No comments