AUDIO: "NATANGA NA NJIA" WIMBO ALLY STAR ANAOKIRI ALIUNYOFOA KWA KING KIKII


JUNI 30, 2015 Saluti5 iliposti malalamiko kutoka kwa mkongwe wa dansi Bongo, King Kikii aliyekuwa akidai kuwa nguli wa mipasho, ambaye aliwahi kuwa mpiga kinanda kwenye bendi yake ya zamani ya “Double O”,  Ally Hemed Star amemuibia wimbo wake ambao ni “Natanga na Njia”.

Katika malalamiko hayo, Kikii alisema kuwa hakuwahi kukirekodi kibao hicho ambacho mwenyewe alikipa jina la “Nanga Natia” na Ally Star akautumia mwanya huo kuchukua kibao hicho cha dansi na kukigeuzia katika miondoko ya taarab.

Wiki hii ikiwa ishapita takriban miaka miwili, Star ameibuka na kukubali kuwa ni kweli alinyofoa kipande cha wimbo huo na kuunda kibao cha “Natanga na Njia” ambacho kilitokea kushika chati kubwa katika miaka ile ya 1995.

“Natanga na Njia” ndiyo iliyobeba albamu yenye vibao sita vingine vikiwa ni “Changudoa”, “Mkate”, “Iam Sorry”, “Asojijua” na “Usinifatefate”, ambapo kwa upande wa washiriki, Said Mpiruka alisimama kwenye gitaa la solo, Hamad Mperembe (rythym) na Khatib Kitia (bass).


Kwenye kinanda cha wimbo huo ambao Ally Star mwenyewe analalamika zaidi akisikitika na umasikini wake, ametulia Juma Jerry “Mzee wa Mbezi”, Patrick Thomas (Drums) na pakashen zimegongwa na Mzee Issa na marehemu Kauzibe.  

No comments