AZAM FC WASISITIZA “LAZIMA TUKIMBIZE LIGI KUU MSIMU HUU”

PAMOJA na uwepo wa majeruhi, Shaaban Idd, Afisa Habari wa klabu ya Azam FC, Jaffar Idd amesema mpango wao wa kurejea kileleni kwenye michuano ya Ligi Kuu  bara uko palepale kutokana na maandalizi ambayo wamefanya mchini Uganda.

Jaffar amesema kwamba imekuwa vyema kuanzia ugenini katika mchezo wao wa kwanza dhidi ya Ndanda kabla ya kumalizia nyumbani wakati wa mzunguuko wa pili kwani kwa hivi sasa kikosi kina hali nzuri baada ya kuweka kambi nchini Uganda.

“Uongozi umempeleka Shabaan nchini Afrika Kusini katika jiji la Pretoria kwa ajili ya kupata matibabu lakini hilo haliwezi kusimamisha mipango yetu ya kukaa kileleni tangu mechi ya kwanza,” alisema Afisa habari huyo.

“Hatutakuwa tena na mechi ya kujipima nguvu baada ya kucheza na kikosi cha vijana cha AzamFC katika uwanja wetu kwasababu sasa nguvu yetu tumeielekeza Mtwara kwenye mechi na Ndanda,” aliongeza.


Azam imepania kurejesha hadhi yake baada ya kukosa nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa kwa kukosa kubeba ubingwa wa Kombe la FA na michuano ya Ligi Kuu bara.

No comments