Habari

BAADA YA NEYMAR KUTUA PSG, BARCELONA SASA YAMWINDA DI MARIA …Coutinho huyoo Camp Nou

on

BAADA ya Neymar kukamilisha
uhamisho wa kujiunga na klabu ya PSG, sasa  Barcelona imeripotiwa
kuelekeza nguvu zao katika kumuwinda Angel Di Maria.
Barcelona wanahaha kusaka
mshambuliaji mwingine wa nguvu ili kuziba pengo la Neymar aliyetua nchini
Ufaransa na wanaona Di Maria anayeitumikia PSG kama chaguo sahihi.
Klabu hiyo imepanga kukamilisha
usajili huo kabla ya dirisha la usajili halijafungwa.
Hata hivyo Barcelona wako mbioni kumalizana na mshambuliaji wa Liverpool, Philippe Coutinho hatua ambayo inaweza ikazima mipango ya kusaka saini ya Di Maria.
Tetesi zinadai Barcelona tayari wamekubaliana na Liverpool juu ya uhamisho wa Coutinho kwa pauni milioni 108.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *