BABA MZAZI WA KICHANGA CHA HAMISA MOBETTO NI KITENDAWILI KIGUMU

MODO na mpambaji wa video za wanamuziki Bongo, Hamisa Mobetto amejifungua huku baba mzazi wa mtoto huyo akiwa bado ni fumbo kwa mashabiki wa muziki wa kizazi kipya.

Taarifa zisizokuwa rasmi zinadai kuwa mtoto huyo ni wa Diamond Platinumz ambaye anaishi na mfanyabiashara wa Uganda, Zari.

Hata hivyo katika moja ya mahojiano na mama mzazi wa Hamisa katika kituo kimoja cha habari hapa nchini, yaliashiria kuwa familia hiyo haitaki kuweka wazi jina la baba mzazi wa mtoto huyo.


"Nikusaidie nini tunaendelea salama na mtoto mchanga na mama yake mzima pia, alijifungua kawaida," alisema mama mzazi wa Hamisa.

No comments