BADO SIKU TATU TU "USIKU WA KUCHARUKA KIPWANI" DAR LIVE

ILE shoo bab kubwa iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki wa mipasho, iliyopewa jina la ‘Usiku wa Kucharuka Kipwani na Singeli’ imewadia.

Shoo hiyo inatazamiwa kupigwa siku tatu tu zijazo, yaani Jumamosi hii ndani ya Dar Live, Mbagala Zakheem, jijini Dar es Salaam kuanzia majira ya saa 3:00 usiku na kuendelea hadi majogoo.
Bendi mbili zinazotesa katika anga la mipasho hivi sasa za Jahazi Modern Taarab na Zanzibar Stars zitatumbuiza jukwaa moja, huku wasanii Khadija Kopa, Khadija Yussuf, Hanifa Maulid, Dullah Makabila na Kivurande Junior wakisindikiza.


Mashabiki wote wa burudani jijini Dar es Salaam wameombwa kujitokeza kwa wingi katika shoo hii ambayo kiingilio chake kimepangwa kuwa sh. 7,000 na ambayo hadi sasa imejaa msisimko mkubwa.

No comments