BARCELONA YAKARIBIA KUWANASA COUTHINHO NA DEMBELE KWA PAUNI MIL 180



Mtendaji mkuu wa Barcelona Pep Segura amefichua kuwa mpango wao wa pauni milioni 180 kwaajili ya kuwanasa Philippe Coutinho na Ousmane Dembele unakaribia kukamilika.

Liverpool imekuwa ikisisitiza kuwa Coutinho hataondoka Anfield licha ya mshamuliaji huyo wa Brazil kuomba uhamisho huku Barcelona ikiwa imeweka mezani pauni milioni 90.

Lakini baada ya kushindwa kutwaa taji la Spanish Super Cup dhidi ya wapinzani wao Real Madrid, Pep Segura amefichua kuwa dili la Coutinho na Dembele liko mbioni kukamilika.

No comments