Neymar hakufanya mazoezi leo na ameruhusiwa kuondoka Barcelona, klabu hiyo imethibitisha.
Taarifa rasmi ya Barcelona imesema: "Neymar amewaambia wachezaji wenzake kuwa anaihama klabu.
"Kocha ameruhusu Neymar kutoshiriki mazoezi ili ashughulikie hatma yake."
Usajili wake wa pauni milioni 196 kwenda Paris Saint Germain unategemewa kukamilika kabla ya mwishoni mwa wiki hii.
Wachezaji wenzake wengi wa Barcelona wamekuwa njia panda wakiwa hawajui ni wapi atakuwepo mwenzao mwanzoni mwa msimu.
USISAHAU KUBONYEZA SUBSCRIBE HAPO
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac