BARCELONA YAWEKA MEZANI PAUNI MIL 114 USAJILI WA COUTINHO, LIVERPOOL YATOA TAMKO


Barcelona imeweka mezani pauni milioni 114.2 ili kumsajili kiungo wa Liverpool Philippe Coutinho.

Hata hivyo habari mbaya kwa miamba hiyo ya Hispania ni kwamba Liverpool imesisitiza mchezaji huyo hauzwi.

Coutinho ameomba klabu yake imruhusu ahame huku Barcelona wakiwa tayari kupanda dau hadi pauni milioni 118, lakini kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp amesema nyota huyo wa kimataifa wa Brazil hataondoka kwa gharama yoyote ile.

No comments