BEKI ERASTO NYONI AANZA MAKEKE SIMBA SC

BEKI wa zamani wa Azam FC, Erasto Nyoni amedhihirisha kuwa wekundu wa Msimbazi, Simba hawakukosea kumsajili baada ya kufungua kaunti ya mabao kwa timu hiyo.

Nyoni akicheza mchezo wake wa pili akiwa amevalia jezi ya Msimbazi alionyesha kiwango cha hali ya juu kwenye mchezo wa kirafiki wa timu hiyo dhidi ya mabingwa wa Afrika Kusini Bidvest Wits.

Beki huyo alionekana kudumu vyema kucheza nafasi ya beki ya kulia na kucheza kwa uelewano mkubwa na wenzake, kiasi cha kumfanya kocha wake Joseph Omog kutabasamu.

Katika mechi hiyo ya katikati ya wiki, Nyoni alionekana kusaidia timu yake katika kupandisha mashambulizi za kuisaidia timu yake kupata bao la mapema kwenye mchezo uliomalizika kwa sare ya bao 1-1.

Simba, ambayo ipo nchini Afrika Kusini takriban wiki tatu, imekuwa ikijiwinda na mechi ya tamasha la Simba Day na ile ya Ngao ya Jamii dhidi ya wapinzani wao wa jadi, Yanga itakayopigwa Agosti 23, mwaka huu kwenye uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Katika tamasha lao la Simba Day Agosti 8, Wekundu wa Msimbazi hao watacheza mechi ya kirafiki na Rayon Sports ya Rwanda huku pia ikitumia nafasi hiyo kutambulisha wachezaji wao wapya iliowasajili msimu huu.


Simba hadi sasa imewasajili wachezaji 13, ambao ni Aishi Manula, Emmanuel Mseja, Said Mohammed, Salim Mbonde, Ally Shomar, Jamal Mwambeleko, Yusuph Mlipili’ Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, Emmanuel Okwi, John Bocco, Nicholas Gyan na Haruna Niyonzima, anayedaiwa kutua Msimbazi, japo hadi sasa bado hajathibitishwa rasmi.

No comments