BERNARDO SILVA ASEMA ANATAMANI KUUNGANA NA MBAPPE MANCHESTER CITY

STAA Bernardo Silva amesema kwamba angependa kuona akiungana  na mwenzake kutoka  AS Monaco, Kylian Mbappe katika kikosi cha Manchester City.

Kwa sasa vinara hao wa Ligi Kuu England, Man  City wapo vitani na timu za  Real Madrid, Barcelona na  Paris Saint-Germain wakimwania straika huyo mwenye umri wa miaka 18 ambaye thamani yake inatajwa kuwa Euro milioni 18.

Msimu uliopita Silva alicheza sambamba na Mbappe  katika timu hiyo ya AS  Monaco amba;po alimshuhudia Mfaransa huyo akicheka na nyavu mara  26 katika mashindano yote yaliyoisaidia pia kutwaa ubingwa wa nchini hiyo  Ligue 1.

 Akizungumza juzi staa huyo aliyesajilima msimu huu  na Man City alisema kuwa ana matuamaini ya kukipiga tena na Mbappe katika kipindi ambacho atakuwa Etihad.

 "Ningependa kuwa naye mahali hapa, lakini Man City ndio wanatakiwa kuamua ," alisema Bernardo.


"Anaweza kuwa supa staa kwa sababu ameshaelekea katika njia hiyo. Nimchezaji mzuri kucheza naye kwa sababu ni jasiri,”aliongeza nyota huyo.

No comments