BEYONCE ASEMA HAJAWAHI KUFIKIRIA KUMDAI TALAKA JAY Z

STAA wa medani ya muziki nchini Marekani, Beyonce, kwa mara ya kwanza ameibuka na kudai kuwa hajawahi kufikiria kudai talaka toka kwa mzazi mwenzie, Jay Z.

Beyonce amesema kwamba kumekuwa na taarifa nyingi zinazomhusisha yeye kutaka kuachana na mzazi mwenzie huku akidai kwamba anafurahi maisha ya ndoa na rapa huyo.

“Nafurahi kuitwa mama bora chini ya rapa Jay Z na sijawahi kifikiria kusihi bila yeye,”alisema dada huyo.

“Nimezaa nae na natarajia kuendelea kuzaa nae kwa sababu nahisi kuwa kuna sehemu yake katika maisha yangu,” aliongeza dada huyo.


Jay Z na Beyonce wamekuwa wakiripotiwa kwenye vyombo vya habari kutaka kuachana tangu mdada huyo akiwa na ujauzito, jambo ambalo kwa mara ya kwanza Beyonce ameibuka na kulikanusha vikali.

No comments