BEYONCE KUNUNUA TIMU YA MPIRA WA KIKAPU

MSANII wa muziki nchini Marekani Bayonce Knowles, anataka kuonesha jeuri ya fedha kwa kuinunua timu ya kikapu ya Houston Rockets ambayo inashiriki Ligi Kuu ya NBA nchini humo.

Mrembo huyo ambaye anakadiriwa kuwa na utajiri wenye thamani ya dola mil 350 ambazo ni zaidi ya bilioni 775 za Kitanzania, ameweka wazi kuwa yupo kwenye mipango ya kuinunua timu hiyo baada ya mmiliki wake, Les Alexander kuthibitisha kuiuza.

Timu hiyo imewahi kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya kikapu nchii humo mara mbili Alexander aliinunua timu kwa kitita cha dola Mil 85 mwaka 1993 zaidi ya Bil 188.


Beyoncwe anataka kufuata nyayo za mume wake Jay Z ambaye aliwahi kuwa hisa katika timu ya Brooklyn Nets lakini alikuja kuziuza mwaka 2013.

No comments