BLAISE MATUIDI MBIONI KUTUA JUVENTUS

VINARA wa soka wa Ligi Kuu nchini Italia, Juventus wamefikia hatua za mwisho kumalizana kiungo wa klabu ya PSG Blaise Matuidi baada ya kumalisha vipimo juzi.

Kiungo huyo anatarajia kusaini mkataba wa kaka mitatu wa kuitumikia klabu hiyo kwa uhamisho wa pauni mil 18 awali alikuwa anahusishwa kutaka kujiunga kwa kitita cha pauni mil 23.

Mchezaji huyo atakuwa wa 10 kujiunga na Juventus katika kipindi hiki cha majira ya joto huku baadhi ya wachezaji wengine waliosajiliwa ni pamoja na Wojciech Szczesny, Douglas Costa na Federico Bernardeschi.


Matuidi alikuwa na mchango mkubwa katika kikosi cha PSG msimu ulipita huku akicheza jumla ya michezo 34 na kufunga mabao mane za mwisho hivyo Juventus wanaamini watapata mafanikio makubwa kupitia usajili huo.

No comments