MKALI wa muziki wa Pop, Britney Spears, ameanza mazoezi kwa kasi ili kuuweka fiti mwili wake, mara baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu na kuwapa wakati mgumu mashabiki wake.

Mwanamama huyo aliweka video katika mtandao wa kijamii wa Instagram, ambapo alionekana akifanya mazoezi mbalimbali ambayo alikuwa akiyafanya kwa ustadi mkubwa.

Mkali huyo mwenye umri wa miaka 35, amerudi kwenye mwonekano wake wa kuvutia mara baada kufanya mazoezi hayo kwa muda wa wiki moja mfululizo.

Mama huyo wa watoto watatu alionekana akipiga 'push up,' kunyanyua vyuma pamoja na mazoezi ya kulainisha viungo, maarufu kama yoga.

"Ni zaidi ya wiki moja sasa. Ni kweli nauweka fiti mwili wangu ambao utaniongezea ushawishi mimi kila siku," aliandika ujumbe huo mara baada ya kuposti video hiyo.
USISAHAU KUBONYEZA SUBSCRIBE HAPO
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac