BRUNO FERNANDES KUZIBA PENGO LA PIZZI TIMU YA TAIFA URENO

SHIRIKISHO la soka nchini Ureno limetangaza kuwa limeamua kumwita kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya nchi hiyo nyota wa timu ya Sporting Lisbon,  Bruno Fernandes  ili aweze kuziba nafasi iliyoachwa wazi na kiungo wa Benifica, Pizzi kwa ajili ya mechi mbili za kufuzu fainali za Kombe la Dunia dhidi ya Visiwa vya Faroe  na  Hungary  ambazo zinatarajiwa kupiga hivi karibuni.

Shirikisho hilo lilieleza jana kwamba staa huyo mwenye umri wa miaka 27 tayari alikuwa ameshajiunga na kikosi hicho cha mabingwa wa Ulaya kinachojiwinda na michezo hiyo mjini  Lisbon, lakini wameamua kumruhusu arejee kikosini kwake baada ya kuomba kufanya hivyo.

Taarifa hiyo ya juzi kutoka katika shirikisho hilo ilieleza kuwa  wameamua kumuita  Fernandes, 22 kutokana na kuonesha kiwango kizuri akiwa na Sporting, baada ya kuitema klabu yake ya zamani ya Sampdoria.

Katika mfululizo wa michuano hiyo, Ureno wataivaa timu ya Taifa ya Visiwa vya Faroe kesho katika Uwanja wa  Estadio do Bessa  uliopo katika mji wa  Oporto kabla ya Jumapili kuivaa  Hungary  mjini  Budapest.

Kikosi kamili cha timu hiyo ni kama ifuatavyo
Walinda mlango: Rui Patricio (Sporting), Beto (Göztepe ), Bruno Varela (Benfica).

Mabeki : Joao Cancelo (Inter Milan ), Cédric Soares (Southampton ), Pepe (Besiktas ), Bruno Alves (Rangers ), José Fonte (West Ham ), Fabio Coentrao (Sporting), Eliseu (Benfica).

Viungo ni : William Carvalho (Sporting), Adrien Silva (Sporting), Danilo Pereira (FC Porto), Joao Moutinho (Monaco ), Bruno Fernandes (Sporting), Joao Mario (Inter Milan ), André Gomes (Barcelona ).


Mastraika : Cristiano Ronaldo (Real Madrid ), Bernardo Silva (Manchester City ), Ricardo Quaresma (Besiktas ), Gelson Martins (Sporting), André Silva (AC Milan ), Bruma (RB Leipzig ), Nelson Oliveira (Norwich ).

No comments