BUZUKI LA ‘WEEK-END BONANZA’ YA CLOUDS FM KUITEKA KIBAHA JUMAMOSI HII …Twanga ndani ya nyumba


Kipindi namba moja cha muziki wa Kiafrika “Week-end Bonanza” cha Clouds FM, Jumamosi hii kitawasha moto wa burudani ndani ya Kibaha.

Weekend Bonanza kupitia ule mpango wake wa buzuki live kutoka kwenye viwanja vya burudani, kitasikika moja kwa moja ndani ukumbi wa River Road Bar, Kibaha Picha ya Ndege kuanzia saa 4 usiku hadi 7 usiku.

Lakini kama vile hiyo haitoshi, Week-end Bonanza inayoongozwa na mtangazaji Khamis Dacota sambamba na Dj Bullah, itapambwa na show ya bendi ya The African Stars “Twanga Pepeta”.

Tayari mzuka wa mashabiki wa dansi umeshika hatamu ambapo Saluti5 imebaini kuwa wanazi wengi wa muziki huo wamepania kwenda Kibaha Jumamosi hii kula buzuki la Week-end Bonanza na Twanga Pepeta.

Kwa wale ambao hawatapata fursa ya kwenda Kibaha, basi wanaweza kupata uhondo huo kupitia Clouds FM kuanzia saa 4 za usiku.


No comments