CANNAVARO ASEMA ANA KIU NA SIMBA AGOSTI 26

BEKI mkongwe wa klabu ya Yanga, Nadir Haroub "Cannavaro" amesema kuwa ana shauku ya kuwepo uwanjani katika pambano la watani wa jadi dhidi ya Simba ambao ni mabingwa wa Kombe la FA hapa nchini.

Cannavaro amesema kuwa shauku ya wachezaji walioko Yanga kwa hivi sasa ni kuona namna ambavyo watawashangaza mashabiki wa Simba katika mchezo wa Kombe la ngao ya hisani.

“Najua namna ambavyo wanajiamini lakini nikwambie ukweli hapa Yanga kila mchezaji ana shauku ya kuinyamazisha Simba katika mechi hiyo,”alisema beki huyo.

Hatuwezi kubeza usajili wao lakini sio jambo linaloweza kututisha kwa sababu tumejiandaa vya kutosha kukabiliana na timu yoyote ile ndani na nje ya nchi,”alimaliza beki huyo.


Simba na Yanga zinatarajia kukutana katika mchezo wa Kombe la ngao ya jamii kabla ya kuanza kwa michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

No comments