CHAMELEONE ATHIBITISHA KUMWAGANA NA MKE WAKE

NYOTA wa muziki nchini Uganda, Jose Chameleone amethibitisha kuachana na mke wake, Daniela Atim na kudai kwamba anafurahi kuishi peke yake kwa sasa.

Mwezi mmoja uliopita kwenye mtandao wa kijamii kulikuwa na taarifa kwamba msanii huyo ameachana na mke wake lakini baadaye staa huyo aliwajia juu watu ambao walikuwa wanasambaza habari hizo huku akidai kwamba wanamtafuta ubaya.

Hata hivyo juzi msani huyo alithibitisha kuachana na mama watoto wake huyo huku akisisitiza kwamba kwake ni furaha kuvunjika kwa ndoa hiyo.


“Nina furaha kuwa "Singo", tena nashukuru sana kwa kipindi ambacho nimekaa na wewe kwenye ndoa, pia naomba radhi kwa kukupotezea muda wako kwa kipindi chote hicho cha miaka tisa ya ndoa, siku zote nitakukumbuka. Najua nimefanya mengi mabaya kuliko mazuri, nisamehe kikubwa ni kuwalea watoto wetu vizuri,” alisema Chameleone.

No comments