CHAZ BABA ASEMA MSHIKO MKUBWA ZAIDI WA JUKWAANI ALIUPATA TWANGA PEPETA


Mwimbaji Chaz Baba aliyetesa zaidi na bendi za The African Stars “Twanga Pepeta” na Mashujaa Band, amefichua ni wapi aliwahi kutuzwa mshiko mrefu zaidi jukwaani.

Chaz Baba akiongea na kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM, leo mchana, akasema anakumbuka ni enzi alizokuwa akiitumikia Twanga Pepeta ndipo alipata pesa nyingi zaidi.

“Nakumbuka ilikuwa Jumatano fulani wakati naitumikia Twanga Pepeta, ndani ya Club Bilcanas, nilitunzwa kama milioni mbili na laki tatu jukwaani,” alisema Chaz Baba.

No comments