CHAZ BABA NDANI YA MAPACHA MUSIC BAND LEO USIKU CLUB MASAI KINONDONI


Mmoja wa waimbaji bora kabisa wa muziki wa dansi Chaz Baba, leo usiku atajitosa kwenye jukwaa la Mapacha Music Band chini ya Jose Mara.

Hiyo itakuwa ni ndani ya ukumbi wa Meridian Hotel (Club Masai) Kinondoni ambapo Chaz Baba atakuwa ni msanii mwalikwa.

Jose Mara ameiambia Saluti5 kuwa Chaz Baba amealikwa katika onyesho ili kuongeza ladha tofauti pamoja kukuza udugu baina ya wasanii wa dansi.

Mapacha Music Band kwasasa inaendelea kutesa na wimbo wao mpya “Dunia Simama”.

No comments