CHICHARITO AKATAA KUFUNGUKA NAMNA ATAKAVYOSHEREHEKEA BAO LAKE DHIDI YA MAN UNITED JUMAPILI

STRAIKA wa zamani wa Manchester United, Javier Hernandez amekataa kuweka wazi kama ataweza kushangilia endapo ataifungia bao timu yake ya sasa West Ham wakati zitakapokutana kwenye Uwanja wa Old Trafford.

 Hernandez atarejea jijini Manchester, Jumapili ijayo katika mchezo wake wa kwanza wa Ligi Kuu England msimu huu lakini akiwa katika jezi  yenye rangi ya zambalau na bluu baada ya kujiunga West Ham akitokea kwenye klabu inayioshiriki Ligi Kuu ya Ujerumani, Bundesliga, Bayer Leverkusen.

Staa huyo mwenye umri wa miaka  29 raia wa  Mexico aliondoka Man United  miaka miwili iliyopita na kwenda kujiunga na  Leverkusen ambako nako alishindwa kufanya vyema, baada ya kufunga mabao 50 katika mashindano yote.

Hata hivyo  Hernandez anasema kuwa hana uhakika jinsi hali itakavyokuwa endapo atafanikiwa kufungua akaunti yake ya mabao akiwa kwenye klabu hiyo mpya ya West Ham katika mtanage huo wa mwishoni mwa wiki.

"Siwezi kufahamu kama nitashangilia endapo nitafunga baoa nikiwa Old Trafford," alisema nyoya huyo.


"Ni klabu yangu ya zamani,mashabikiwa wa zamani, uwanja wangu wa zamani,lakini litakuwa ni bao langu la kwanza kwa  West Ham,”aliongeza staa huyo.

No comments