CHRIS BROWN AKIRI MCHEPUKO ULIMPONZA KUMKOSA RIHANNA

RAPA Chriss Brown amefunguka kwa mara ya kwanza akikiri kuwa penzi lake na Rihana lilikufa tangu dada huyo mrembo alipogundua jamaa alichepuka.

Chriss amesema kuwa suala la yeye kutengana na Rihana halikutokana na kipigo alichompa kwani tayari walishatengana kwasababu ya mchepuko.

“Rihana alipoteza uaminifu kwangu akawa anafanya kile anachojisikia yeye, ilikuwa tunaishi kama watu waliopo kwenye penzi moja,” alisema staa huyo.

“Nilijaribu kufanya kila namna kumbadilisha ilishindiana, nadhani aliamua kunihukumu kwa kile nilichofanya,” aliongeza.

“Hata suala la mmi kugombana nae lilikuzwa sana na vyombo vya habari lakini hakuna aliyekuwa anajua mwenendo wa penzi letu siku za nyuma,” alimaliza.

     

No comments