CHRISTIAN BELLA KUIFUMUA NGOME YA ‘KIINGILIO KINYWAJI’ JUMAMOSI HII BL PARK TABATA KINYEREZI


Jumamosi hii Agost 19, pande za Tabata Kinyerezi litafanyika onyesho kubwa la mfalme wa masauti Christian Bella akiwa na bendi yake ya Malaika ndani ya kiota cha maraha cha BL Park.

Hapo BL Park ndipo pale ambapo bendi zote zilizotia mguu zikiwemo FM Academia na Twanga Pepeta, ziliishia kupiga show za kiingilio kinywaji.

Lakini kumuona Bella na Malaika Band, mshabiki atalazimika kulipa shilingi elfu 10,000 kwa viti kawaida au shilingi 20,000 kwa sehemu ya V.I.P.

Mratibu wa onyesho hilo Issa Mwendapole ameiambia Saluti5 kuwa watabadilisha kabisa madhari ya BL Park kwa kuzungusha uzio mkubwa, jukwaa la kisasa, mapambo bab kubwa, unadhifu pamoja na ‘sound’ si ya kitoto.

Mwendapole amesema onyesho hilo ni maalum kwaajili ya utambulisho wa nyimbo tatu mpya za Bella “Shuga Shuga”, “Niende Wapi” na “Punguza Kidogo” ambazo bado hazijaachiwa hewani.

No comments