Habari

CHUJI AREJEA LIGI KUU KWA KUJIUNGA NA NDANDA FC

on

ATHUMANI Idd “Chuji” amerejea Ligi Kuu bara baada ya kujiunga na
Ndanda FC ya Mtwara.
Chuji amerejea kwa kusaini mkataba wa mweaka mmoja kuichezea
Ndanda ambayo msimu uloipita ilifanya kazi ya ziada kubaki Ligi Kuu Bara.
Kiungo huyo wa zamani wa Yanga alipotea baada ya kuachwa na
Yanga misimu mitano iliyopita.
Juhudi zake za kutaka kurejea Ligi Kuu Bara zilionyesha kutokuwa
na mafanikio hata alipojiunga na Mwadui FC ya Shinyanga ambayo licha ya kukaa
misimu miwili, hakupata nafasi ya kucheza.

Baada ya hapo Chuji aliamua kijiweka kando mwa Ligi hiyo na hivi
karibuni alii buka na kufanya vizuri katika michuano ya Ndondo FC.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *