COUTINHO AANZA KUITINGISHA LIVERPOOL... adai kutaka kusepa zake Barcelona

FHILIPPE Coutinho sasa ameanza kuitikisa klabu ya Liverpool akisema anataka kuondoka zake aende Barcelona.

Barcelona inamtaka mchezaji huyo kwa ajili ya kuziba nafasi ya Neymar aliyemtimkia PSG ya Ufaransa kwa dau nono la pauni mil 198.

Klabu hiyo imesema kuwa mchezaji huyo ndiye anayetakiwa zaidi na inaonekana kuwa ndiye mrithi wa Neymar katika safu ya mshambuliaji wa hao wa Camp Nou.

Pamoja na mikwara hiyo, kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp amesema kuwa kuwa hana mpango wa kumwachia Coutinho aondoke.

No comments