COUTINHO AZIDI KUNUKIA BARCELONA

STRAIKA wa Liverpool, Phillipe Coutinho, anakaribia kutua Barcelona baada ya vinara hao wa soka Hispania kudaiwa kufikia makubaliano binafsi na staa huyo.

Taarifa kutoka Hispania zilieleza juzi kuwa mbali na mchezaji, klabu hizo mbili za Liverpool na Barcelona nazo zinaelekea kufikia makubaliano na huku Reds nao wakiwa wameshamtaka Mbrazil huyo kuwaweka wazi kama atakuwa nao kufikia Agosti mwaka huu.

No comments